Wednesday, 17 May 2017

Guardiola: Nisingeshinda kombe, Barcelona na Bayern wangenifuta

Meneja wa Manchester City Pep Guardiola
Meneja wa Manchester City Pep Guardiola amesema angekuwa amepigwa kalamu na klabu zake za hapo awali za Barcelona na Bayern Munich kama angekamilisha msimu bila kupata kikombe chochote.
City imeshindwa kupata ushindi tangu Guardiola alipoanza kuiongoza mwanzo mwa msimu huu, na hawana uhakika kumaliza katika nafasi nne bora katika ligi ya Premia licha ya kusalia na mechi mbili.
Upande wa Guardiola ulipoteza katika hatua ya timu 16 bora katika ligi ya klabu bingwa ulaya ,nusu fainali ya kombe la FA na kombe la ligi katika raundi ya nne.
"Katika hali yangu katika klabu kubwa , Ningefutwa. Ningetoka," Amesema mhispanio huyo.
Ingekuwa ni Barcelona au Bayern kukosa kushinda basi utatolewa. Hapa nina nafasi ya pili na nitajikaza kufanya vyema msimu ujao.
City wanahitajika kupata ushindi katika fainali ya mchezo wa ligi ili kujipatia nafasi ya tatu mbele ya Liverpool na Arsenal ili wapate tiketi ya moja kwa moja kujiunga na msimu ujao katika ligi ya Champions.


Watawakaribisha nambari nane West Brom siku ya Jumanne kabla safari yao ya Jumapili kuelekea Watford ambao wako katika nafasi ya 16.Jeduali ya timu sita bora katika ligi ya PremiaMhispania huyo aliyechukua nafasi ya Manuel Pellegrini msimu uliopita, alikuwa na matumaini makubwa baada ya kutoka katika timu za Barcelona na Bayern akiwa na matarajio makubwa.
Kiungo huyo wa kati wa zamani wa Barcelona mwneye umri wa miaka 46, aliongoza Catalan kujinyakulia vikombe 14 kwa miaka 4 ikijumuisha kushida taji mara tatu ligi ya La Liga na mara mbili ligi ya Champions katika mwaka 2008 na 2012.
Baada ya mapumziko ya mwaka mmoja , alijiunga na klabu kubwa ya Ujerumani ya Bayern mwaka 2013 na kushinda ligi ya Bundesliga katika misimu yote mitatu aliyoiongoza katika uwanja wa Allianz Arena
Bayern pia ilishinda kombe la Ujerumani mara mbili wakati huo lakini Guardiola hakuweza kuowaongoza kufuzu katika nusu fainali ya ligi ya klabu bingwa ulaya.
Mashabiki wa City walitumai kuwasili kwake, kutawapatia ushindi wao wa kwanza katika ligi ya Premia katika misimu mitatu, licha ya kushinda mechi sita za ufunguzi , wamepata changamoto nyingi za kumaliza katika nafasi ya timu nne bora.
Arsenal ambao wako katika nafasi ya tano wanamatumaini kuchukua nafasi iwapo City itashindwa kupata alama katika michuano yao miwili, Lakini Guardiola amempuzilia mbali meneja wa Gunners Arsene Wenger kwamba ''timu nyengine ziko likizoni.''
''Sijawahi kumuona hata mchezaji mmoja maishani mwangu akienda uwanjani bila ya kujaribu kupata ushindi, alisema.
Arsenal itacheza dhidi ya Sunderland na Everton ambayo moja imeshushwa daraja na moja iko katika ligi ya bara ulaya kwa hivyo iko katika hali sawa.

Waziri wa zamani afaulu mtihani akiwa na miaka 82 India

Bw Chautala alihudumu kama waziri mkuu wa jimbo la Haryana kaskazini mwa India kwa mihula minneWaziri wa zamani ambaye anatumikia kifungo gerezaji baada ya kupatikana na kosa la kula rushwa amefaulu mtihani wa kumaliza shule India akiwa na miaka 82.
Om Prakash Chautala, aliyehudumu kama waziri mkuu wa jimbo la Haryana kaskazini mwa India kwa mihula minne, alifanya mtihani wa darasa la 12 akiwa katika jela ya Tihar mjini Delhi.
Mwanawe wa kiume Abhay Chautala alisema babake aliamua "kutumia vyema muda wake gerezani".
OP Chautala alipatikana na makosa kuhusiana na kuajiriwa kwa walimu.
Abhay Chautala aliambia gazeti la Indian Express kwamba babake amekuwa kila siku akienda kusoma katika maktaba ya gereza hilo.
"Husoma magazeti na vitabu. Huwa anawaomba wafanyakazi wa jela kumtafutia vitabu avipendavyo zaidi. Husoma vitabu kuhusu wanasiasa maarufu duniani,2 amesema.
Bw Chautala na 54 wengine, walipatikana na hatia ya kughushi vyeti walipokuwa wanwaajiri walimu 3,206 kati ya 1999 na 2000.
Waendeshaji mashtaka walisema watu waliokuwa wamehitimu zaidi walikataliwa na badala yake wale waliokuwa wametoa hongo wakaajiriwa.
Bw Chautala ni kiongozi wa chama cha Indian National Lok Dal Party na ni mwana wa aliyekuwa naibu waziri mkuu Devi Lal.

Kiongozi wa zamani wa FBI kuchunguza iwapo Urusi iliingilia uchaguzi wa Marekani Saa moja iliyopita Hivi ni viunganisho vya nje na vitafungua katika dirisha mpya Sambaza habari hii Facebook Sambaza habari hii Twitter Sambaza habari hii Messenger Sambaza habari hii Email Mshirikishe mwenzako


Robert Mueller aliingoza FBI kuanzia 2001 - 2013Wizara ya sheria nchini Marekani, imetangaza kuteuliwa kwa mwendesha mashtaka maalum atakae ongoza uchuguzi wa tuhuma kwamba Urusi iliingilia uchaguzi wa marekani wa mwaka jana.
Mwendesha mashtaka huyo aliwahi kuwa mkuu wa shirika la kijajusi la FBI, Robert Mueller.
Pia katika uchunguzi wake, atazingatia iwapo kulikuwa na mwingiliano wa aina yoyote kati ya Urusi na timu ya kampeni ya Trump.
Taarifa iliyotolewa na wizara ya sheria nchini humo imesema uchunguzi huo utaongozwa na mtu asiyeegemea upande wowote kwa ajili ya maslahi ya umma.
Tangazo hilo linafuatia utata uliogubikwa kufuatia kufutwa kazi kwa wiki moja iliyopita kwa James Comey, ambae ndie aliyekuwa akiongoza uchunguzi huo.